TAASISI YA MSIKILIZE MSAIDIE ANAWEZA,YAWATAKA WAZAZI IWALINDE WATOTO NA VITENDO VYA UKATILI, WATIMIZE NDOTO ZAO KATIKA MAISHA YAO,MTOTO ANAPOKUITA ITIKA KWA UPOLE MSIKILIZE PENGINE ANAJAMBO LINAHITAJI MWONGOZO WAKO,SAUTI YAKO YA UKALI INAMUANGAMIZA MTOTO WAKO.
Posts
Showing posts from July, 2021
WATOTO WENYE ULEMAVU TUTAWAWEKA WAPI
- Get link
- X
- Other Apps
Na: Raphael Mwazyunga Changamoto ya wazazi au jamii ya kuwaficha watoto wenye ulemavu inaonekana bado kupatiwa ufumbuzi katika familia zilizonyingi na hii inatokana na mazingira yasiyo rafiki kuanzia majumbani. Watoto wenye ulemavu hukosa fulsa za kielimu,ibada hata michezo kutokana na majengo au viwanja vilivyo na kusahaulika kwa wenye ulemavu Naamini wazazi wengi wanatamani watoto wao wapate elimu,washiriki michezo,waende kwenye Ibada,changamoto iliyopo ninamna ya kusaidia au kwenda chooni kujisaidia. Makanisa,Misikiti hata shule zilizonyingi zimejengwa pasipokuwa na vyoo maalum kwa wenye ulemavu,hivyo mwenye ulemavu hawezi kufurahia au kuipenda huduma hiyo. Wapo walemavu wenye ulemavu wa miguu kukosa nguvu kiasi cha kushindwa kusimama au kuchuchumaa pasipo msaada wa kushikiliwa na mwingine. Ama mzazi au mlezi itampasa ashinde na yeye shule kumsubiri mtoto huyo kumsaidia anapohitaji kwenda msalani. Kwa changamoto hizi wazazi wengi huishia kuwafungia ndani...