Posts

MAJUKUMU YETU YASITUTENGE NA WATOTO WETU

Wazazi wamekumbushwa kutojisahau na kukaa mbali na watoto wao,kwani kufanya hivyo kumeleta changamoto nyingi za malezi kwa watoto. Watoto wengi wamekuwa wakijenga kibuli kwa walezi walio nyumbani baada ya kuona hawana maamuzi juu yao. Hivyo imefanya watoto kuwa wakaidi na watukutu na kujiunga na makundi hatalishi,wapo ambao muda wa kuwa shule wamekuwa wakienda maeneo ya starehe,na hata wakiambiwa wawaite wazazi wao wafike shule hawafanyi hivyo,au ulazimika kuwatafuta watu baki. Wazazi katika siku saba za wiki mtoto hukutana nae siku moja napohukosa muda wa kuongea na mtoto.
 TAASISI YA MSIKILIZE MSAIDIE ANAWEZA,YAWATAKA WAZAZI IWALINDE  WATOTO NA  VITENDO VYA UKATILI, WATIMIZE NDOTO ZAO KATIKA MAISHA  YAO,MTOTO ANAPOKUITA ITIKA KWA UPOLE MSIKILIZE PENGINE ANAJAMBO LINAHITAJI MWONGOZO WAKO,SAUTI YAKO YA UKALI INAMUANGAMIZA MTOTO WAKO. 

WATOTO WENYE ULEMAVU TUTAWAWEKA WAPI

 Na: Raphael Mwazyunga  Changamoto ya wazazi au jamii ya kuwaficha watoto wenye ulemavu inaonekana bado kupatiwa ufumbuzi katika familia zilizonyingi na hii inatokana na mazingira yasiyo rafiki kuanzia majumbani. Watoto wenye ulemavu hukosa fulsa za kielimu,ibada hata michezo kutokana na majengo au viwanja vilivyo na kusahaulika kwa wenye ulemavu  Naamini wazazi wengi wanatamani watoto wao wapate elimu,washiriki michezo,waende kwenye Ibada,changamoto iliyopo ninamna ya kusaidia au kwenda chooni kujisaidia.  Makanisa,Misikiti hata shule zilizonyingi zimejengwa pasipokuwa na vyoo maalum kwa wenye ulemavu,hivyo mwenye ulemavu hawezi kufurahia au kuipenda huduma hiyo. Wapo walemavu wenye ulemavu wa miguu kukosa nguvu kiasi cha kushindwa kusimama au kuchuchumaa pasipo msaada wa kushikiliwa na mwingine.  Ama mzazi au mlezi itampasa ashinde na yeye shule kumsubiri mtoto huyo kumsaidia anapohitaji kwenda msalani. Kwa changamoto hizi wazazi wengi huishia kuwafungia ndani...