WATOTO WENYE ULEMAVU TUTAWAWEKA WAPI
Na: Raphael Mwazyunga
Changamoto ya wazazi au jamii ya kuwaficha watoto wenye ulemavu inaonekana bado kupatiwa ufumbuzi katika familia zilizonyingi na hii inatokana na mazingira yasiyo rafiki kuanzia majumbani.
Watoto wenye ulemavu hukosa fulsa za kielimu,ibada hata michezo kutokana na majengo au viwanja vilivyo na kusahaulika kwa wenye ulemavu
Naamini wazazi wengi wanatamani watoto wao wapate elimu,washiriki michezo,waende kwenye Ibada,changamoto iliyopo ninamna ya kusaidia au kwenda chooni kujisaidia.
Makanisa,Misikiti hata shule zilizonyingi zimejengwa pasipokuwa na vyoo maalum kwa wenye ulemavu,hivyo mwenye ulemavu hawezi kufurahia au kuipenda huduma hiyo.
Wapo walemavu wenye ulemavu wa miguu kukosa nguvu kiasi cha kushindwa kusimama au kuchuchumaa pasipo msaada wa kushikiliwa na mwingine.
Ama mzazi au mlezi itampasa ashinde na yeye shule kumsubiri mtoto huyo kumsaidia anapohitaji kwenda msalani.
Kwa changamoto hizi wazazi wengi huishia kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu,na watoto wenyeulemavu kukosa fulsa za kukosa elimu na kushirikiana na wenzao,changamoto ya vyoo maalum hata kwenye nyumba huwasahau watoto au watu wenye ulemavu.
Taasisi ya Msikilize Msaidie Anaweza (MMA) imeliona hili baada ya kutembelea Shule ya msingi Karakata iliyopo Kata ya Kipawa, na kuwakuta wanafunzi wakike wawili wenyeulemavu wa miguu shuleni hapo,wanafunzi hawa inawalazimu kukatisha masomo ya siku na kupelekwa nyumbani kwao kwa ajili ya kujisaidia.
Kwa hali hii wanafunzi hawa hawawezi kufanya vizuri katika masomo yao na hatimae wanaweza kuishia njia,kwa wazazi au walezi kuchoka kuwafuata watoto na kuwapeka nyumbani kwaajili ya kwenda msalani,shule haina choo cha wenyeulemavu
Taasisi ya Msikilize Msaidie Anaweza inakuomba kuungana nayo kuchangia kujenga vyoo vya wenye ulemavu,njoo tuanze na shule ya msingi Karakata iliyopo Kata ya Kipawa jijini Dar Es Salaam
Comments
Post a Comment