TAASISI YA MSIKILIZE MSAIDIE ANAWEZA,YAWATAKA WAZAZI IWALINDE WATOTO NA VITENDO VYA UKATILI, WATIMIZE NDOTO ZAO KATIKA MAISHA YAO,MTOTO ANAPOKUITA ITIKA KWA UPOLE MSIKILIZE PENGINE ANAJAMBO LINAHITAJI MWONGOZO WAKO,SAUTI YAKO YA UKALI INAMUANGAMIZA MTOTO WAKO.
MAJUKUMU YETU YASITUTENGE NA WATOTO WETU
Wazazi wamekumbushwa kutojisahau na kukaa mbali na watoto wao,kwani kufanya hivyo kumeleta changamoto nyingi za malezi kwa watoto. Watoto wengi wamekuwa wakijenga kibuli kwa walezi walio nyumbani baada ya kuona hawana maamuzi juu yao. Hivyo imefanya watoto kuwa wakaidi na watukutu na kujiunga na makundi hatalishi,wapo ambao muda wa kuwa shule wamekuwa wakienda maeneo ya starehe,na hata wakiambiwa wawaite wazazi wao wafike shule hawafanyi hivyo,au ulazimika kuwatafuta watu baki. Wazazi katika siku saba za wiki mtoto hukutana nae siku moja napohukosa muda wa kuongea na mtoto.
Comments
Post a Comment